Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, Hafla hiyo ya kipekee, iliyokusanya viongozi mbalimbali wa Kidini na kisiasa pamoja na wageni mashuhuri, imefanyika katika mazingira ya kuimarisha mshikamano, maelewano na uhusiano mwema baina ya viongozi wa dini na jamii kwa ujumla.
Mgeni rasmi katika hafla hiyo alikuwa ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, ambaye aliongozana na viongozi wengine mbalimbali walioshiriki katika maadhimisho hayo.
Ushiriki wa Maulana Sheikh Hemed Jalala Mwakindenge, katika hafla hiyo unaendelea kuonesha umuhimu wa mawasiliano na ushirikiano baina ya viongozi wa madhehebu na taasisi mbalimbali za kidini katika kuimarisha umoja, upendo na kuishi kwa amani miongoni mwa jamii.
Maulid ya Mabohora ni miongoni mwa matukio yanayowakutanisha waumini na viongozi mbalimbali, ikiwa pia ni fursa ya kudumisha uhusiano wa kijamii na kuendeleza misingi ya kuheshimiana na mshikamano.



Maoni yako